RC Akiapishwa

Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Mhe. Mrisho Gambo.

Ziara ya Waziri Mkuu wa Tanzania

Mhe. Mrisho Gambo akiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa Ofisini kwake, Jijini Arusha.

JPM ,Mrisho Gambo Picha ya Pamoja

Dk. John Pombe Magufuli akipiga picha ya pamoja na mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.

Samia Suluhu Hassan akiwasili Jijini Arusha

Mkuu wa Mkoa Arusha, Mhe Mrisho Gambo Akimpokea Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Picha ya Pamoja

Mhe. Mrisho Gambo akiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa.

Friday, January 5, 2018

BILIONI 2 ZATUMIKA KUBORESHA SEKTA YA AFYA

Baadhi ya mafundi wakiwa kazini kwenye ujenzi wa kituo cha afya Nduruma,wilayani Arusha.
Katika kutekeleza maelekezo ya uboreshaji  na  ukarabati wa vituo vya afya nchini, Mkoa wa Arusha amefanikiwa kuboresha vitua vya afya viwili kwa awamu ya kwanza.


Akitoa taarifa fupi ya maendeleo ya ujenzi wa vituo hivyo,Mganga mkuu wa Mkoa Dr.Vivian Timothy Wonanji, amesema mpaka sasa kwa mkoa wa Arusha zoezi hili linaendelea vizuri na kwakasi kubwa.

Awamu ya kwanza, Mkoa ulipata kiasi cha bilioni 1.4 kwa ujenzi wa vituo viwili vya afya,ambapo ni kituo cha afya cha Nduruma kilipata kiasi cha shilingi milioni 500 kwaajili ya ujenzi na milioni 200 kwaajili ya ununuzi wa vifaa na kituo cha afya cha Kambi ya Simba kimepata milioni 500 kwaajili ya ujenzi na milioni 200 za ununuzi wa vifaa.


Amesema kituo cha fya cha Nduruma kilichopo katika halmashauri ya Arusha kinaendelea na ujenzi wa majengo matano na mpaka sasa yapo katika hatua ya ukamilishaji,majengo hayo yakiwemo wodi ya wazazi na jengo la upasuaji.


Kituo cha pili ni Kambi ya Simba kilichopo katika Wilaya ya Monduli, ambapo mpaka sasa ujenzi unaendelea wa majengo nane yakiwa kwenye hatua ya upauwaji.

Aidha,amesema katika awamu ya pili ya ujenzi wa vituo vya afya, mkoa wa Arusha umeshaanza maandalizi yake kwa uundaji wa kamati mbalimbali zakusimamia shughuli nzima na kiasi cha shilingi bilioni 1.2 zimeshatolewa na benki ya dunia kwa ujenzi wa vituo vya afya 3 .

Wilaya ambazo zimepata fedha hizo ni, Wilaya ya Ngorongoro katika ujenzi wa kituo cha afya cha Sakala, Wilaya ya Monduli kituo cha afya cha Mto wa Mbu na Wilaya ya Longido ujenzi wa kituo cha afya cha Engarenaiobor,ambapo kila kituo kitapatiwa kiasi cha shilingi milioni 400.Pia, serikali imetoa fedha za ukarabati wa vituo vya afya mkoani Arusha, kikiwemo kituo cha afya cha Murieti,kimepata kiasi cha milioni 700.
                                                                
Kituo vingine ni kituo cha afya cha Usa liver ambacho kimepata kiasi cha shilingi milioni 700 kwaajili ya ukarabati wa chumba cha upasuaji kwa wakinamama.

Kituo cha afya cha Ololiendeki wilayani Longido nacho kimepata kiasi cha milioni 700 kutoka serikalini.
 
Dokta Wonanji amesema, mpango huu wa ukarabati wa vituo vya afya kwa mkoa wa Arusha, awamu ya kwanza vituo  vya afya 2 vimeweza kunufaika, na awamu ya pili utakamilishwa kwa ukarabati wa vituo vya afya 6 na kupelekea mpango huu kukarabati vituo vya afya 8 kwa mkoa mzima wa Arusha.

Mpango huu wa ukarabati wa vituo vya afya upo katika awamu mbili,yakwanza ilianza rasmi Septemba,2017 na utakamilika Januari,2018,ambapo awamu ya pili umeanza Januari 2,2018 na utakamilika Aprili,2018.


Wednesday, December 20, 2017

Shule binafsi za Sekondari zatakiwa kufuata sheria ya elimu.

Katibu Tawala Msaidizi upande wa elimu akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani)juu ya usimamizi wa sheria ya elimu kwa shule binafsi.


Shule zote binafsi za mkoa wa Arusha zimetakiwa kufuata sheria  ya elimu ya mwaka  2012 ya usimamizi wa upandaji wa madarasa  kwa wanafunzi wa shule hasa  za Sekondari.

Akitoa rai hiyo katibu tawala masaidizi upande wa elimu bwana Gift Kyando, amesema serikali  imeweka utaratibu wa upimaji wa wanafunzi kwa darasa la nne, darasa la saba,kidato cha pili na kidato cha nne.

“Hakuna utaratibu wakumpima mwanafunzi wa kidato cha tatu kwenda kidato cha nne kama inavyofanywa na baadhi ya shule binafsi kwa kuweka wastani wa alama za masomo kwa wanafunzi na ambae hata fikisha kiwango hicho hufukuzwa shule au kuamliwa kurudia kidato”.

Amesema serikali haitafumbia macho kwa shule yoyote itakayokiuka sheria hiyo ya elimu nakuwataka wakuu wote wa shule wanaoendesha shule zao kwa kukiuka utaratibu huo kuacha mara moja na pia amewasihi wazazi wote waendelee na maandalizi ya watoto wao wanaoingia kidato cha nne bila hofu yoyote.

Pia amesema serikali itaendelea kuzifuatilia shule zote za binafsi hasa zilizobainika kukiuka sheria hiyo ili kuhakikisha wanafunzi hawafukuzwi au kurudia madarasa bila utaratibu uliowekwa na serikali.

Amewataka wazazi wote ambao watoto wao watakataliwa kuendelea na masomo kwa kigezo cha kikosa wastani wa alama za shule husika, watoe taarifa haraka katika ofisi za elimu za  mkoa wa Arusha  kwa hatua zaidi.

Friday, August 11, 2017

Katibu Mkuu TAMISEMI Eng.Musa Iyombe ateta na watumishi wa umma wa mkoa wa Arusha.

Katibu Mkuu TAMISEMI,Eng.Musa Iyombe,akizungumza na katibu tawala mkoa Richard Kwitega(kushoto) na katibu tawala wilaya ya Arusha David Mwakiposi(kulia) baada ya kikao na watumishi wa mkoa wa Arusha.

Baadhi ya watumishi wa umma wa mkoa wa Arusha,waliohudhuria kikao cha Katibu Mkuu TAMISEMI,Eng. Musa Iyombe(hayupo pichani) katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa,jijini Arusha.

Friday, July 28, 2017

TIMU YA RIADHA YA TAIFA YAAGWA RASMI MKOANI ARUSHA

Katinu Tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega,akiwa kwenye picha ya pamoja na timu ya riadha ya taifa, jijini Arusha.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega,akikabidhi fedha kwa kocha wa timu ya riadha ya Taifa alipokuwa akiiaga rasmi kwa ajiri ya safari ya London.Timu ya riadha ya taifa imekabidhiwa kiasi cha shiling laki tano kutoka  ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha kama mchango wakuiunga mkono timu hiyo na kuitakia kila la kheri katika mashindano ya dunia.

Akitoa zawadi hiyo katibu tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega amesema, mkoa umeguswa sana na juhudi zinazooneshwa na timu hiyo katika mashindano mbalimbali hivyo kupitia ofisi yake imetoa kiasi hicho ili kuwaunga mkono wanariadha hao.

“Ofisi ya mkoa imeona haitakuwa sahihi sana kuiacha timu hii iondoke hivi hivi bila yakuitakia kheri ya mafanikio katika mashindano hayo ya riadha ambayo niya dunia, wakati imeweka kambi mda wote katika mkoa huu”.

Amewahasa kuwa wanapotoka hapo wawe na mawazo ya ushindi tu na wakazingatie yale yote waliyofundishwa wakati wakiwa kambini na walimu wao.

Aidha, amewataka wanaobaki kambini waendelea na mazoezi kwa juhudi zaidi na wasife moyo kwani mashindano yoyote yanaitaji juhudi na nidhamu ya hali ya juu.

Akitoa salamu za shukrani mmoja wa washiriki wa timu ya taifa Alex Siumbu amesema anaamini wanaenda kushinda na si vinginevyo kwani wameweza kufanya mazoezi kwa mda mrefu na watanzingatia maelekezo yote waliyopewa na walimu wao.

Timu hiyo ya riadha yenye washiriki 8 inatarajiwa kuondoka jijini Arusha Julai 29 kuelekea Dar es Salaama kwa maandalizi yakuangwa kitaifa Julai 31 na kuanza safari yakuelekea London Uwingereza Agosti 1 kwenye mashindano ya dunia.

Baadhi ya wanariadha wa timu ya taifa ya riadha wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha( hayupo pichani) alipokuwa akitoa nasaha za kuwaaga rasmi.

Friday, July 14, 2017

MAANDALIZI YA NANE NANE JIJINI ARUSHA YAMEPAMBA MOTO.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Joel Bendera,akifunga kikao cha maandalizi ya sherehe za nane nane, katika viwanja vya maonyesho hayo,jijini Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Joel Bendera amesema maonyesha ya kilimo na mifugo, maarufu kama nane nane mwaka huu kwa kanda ya Kaskazini yataongoza kwa ubora kwa nchi nzima.


Aliyasema hayo alipokuwa akifunga kikao cha maandalizi ya sherehe hizo za nane nane kwa kanda ya Kaskazini ambayo yanajumuisha mikoa mitatu ya Arusha,Manyara na Kilimanjaro.

Amesema kwa Serikali hii ya awamu ya tano niwajibu wakila mtu kufanya kazi kwa bidii nakuacha kufanyakazi kwa mazoea, ili kila mipango iliyowekwa katika maandalizi hayo yafanikiwe na kanda hii kushika nafasi ya kwanza nakua mfano kwa nchi nzima.

Akisisitiza zaidi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ameziagiza TANESCO na AUWSA kuhakikisha maji na umeme vinapatikana katika maeneo husika ya viwanja vya maonyesho ya nane nane ndani ya wiki moja.

Pia, Gambo amemwagiza mkuu wa wilaya ya Arusha  kuunda tume yakufuatilia taratibu za matumizi ya viwanja hivyo hasa katika wakati ambao sio wa maonyesho, ili kusaidia kupata taarifa kamili itakayosaidia kutoa hali halisi kabla ya makabidhiano baina ya taasisi iliyokuwa ikisimamia maonyesho hayo TASO na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha.

Kaimu mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Gelasius Byakanwa amesema pia katika kikao kijacho nivizuri taarifa ya mapato na matumizi kwa mwaka jana na mwaka huu isomwe kwa wajumbe ili waweze kupata hali halisi ya mapato hayo.

Maonyesho ya nane mwaka huu yataratibiwa na ofisi za makatibu tawala wa mikoa yote mitatu ya kanda ya Kaskazini kwa ushirikiano na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvivu na mpaka sasa ni makampuni  33 tu ndio yamedhibitisha ishiriki katika maonyesho hayo, wananchi wote bado wanahamasishwa kushiriki kuanzia siku ya mwanzo hadi mwisho.


Wakuu wa Mikoa ya kanda ya Kaskazini wakikagua maandalizi ya maonyesho ya nane nane,jijini Arusha.

Baadhi ya viongozi wa kutoka mikoa ya kanda ya Kaskazini waliohudhuria kikao cha maandalizi ya maonyesho ya nane nane,jijini Arusha.

Wednesday, July 12, 2017

ZIARA YA MKUU WA MKOA KATIKA HALMASHAURI YA MERU


Tangazo la Utoaji wa Leseni za Biashara


KATIBU TAWALA,RICHARD KWITEGA ATEMBELEA KITUO CHA SOS CHILDREN VILLAGE

Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega, akiwa pamoja na baadhi ya vijana wanaolelewa katika kituo cha SOS Children Village tokea wakiwa na umri wa miaka 3 na baadhi ya walezi wao,Ngaramtoni.


Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha,Richard Kwitega amesema serikali ipo tayari kutoa ushirikiano wa karibu sana  na taasisi ya SOS Children Village kwenye shughuli wanazofanya hususani zakusaidia watoto wasio na wazazi.

Aliyasema hayo alipotembelea kituo hicho kwa lengo lakutaka kufahamu zaidi namna taasisi hiyo inavyofanya kazi ilikuona nikwajinsi gani serikali inaweza kushirikiana nayo katika kuwalea watoto hao kwakuwa na wao niwatanzania wanahaki zote zakuhudumiwa na serikali yao.

“Serikali ipo tayari kutoa ushirikiano kwa taasisi hii katika maeneo mbalimbali ili kuendelea kutoa huduma iliyo bora kwa watoto wetu hawa na wao waweze kujisikia kweli serikali yao ipo pamoja nao.”

Aidha, amepongeza taasisi hiyo kwa kutoa malezi mazuri kwa watoto hao hasa kwakuwalea kama wapo na wazazi wao halisi hasa kwakuwapa elimu na huduma ya afya.

Bwana Kwitega amesisitiza zaidi kuwa serikali kwa kuanza inaweza kutoa ushirikiano kwa kuleta wataalamu wa elimu yani walimu na wataalamu wa afya ambao watakuwa waajiriwa wa serikali lakini wakitoa huduma katika kituo hicho.

Akitoa historia fupi ya taasisi hiyo,Mkurugenzi wa taasisi hiyo bwana Francis Msollo alisema kituo hicho kilianza mwaka 2000 kikiwa na nyumba 10 tu zakuishi watoto hao lakini mpaka sasa wamefikisha nyumba 15 na watoto 200.

Pia alisema mbali yakuwalewa watoto hao wasio na wazazi, taasisi inatoa pia msaada kwa wale watoto wenye mzazi mmoja kwakuwapa ufadhiri wa elimu inayotolewa katika taasisi hiyo.

Taasisi hiyo pia imetoa nafasi kwa watoto wanaozunguka maeneo ya taasisi hiyo kupata elimu inayotolewa katika kituo hicho.

Akisisitiza zaidi bwana Msollo alisema, Changamoto wanayokabilina nayo kwasasa nikwabaadhi ya wafadhili kujitoa katika kutoa fedha zakutoa huduma za afya na elimu na hivyo kuiomba serikali iangalie naoma yakusaidia taasisi hiyo ili watoto hao waendelee kupata elimu bora na afya.

Msollo amesema, mipango ya baadae ya taasisi hiyo nikuboresha mabweni ya watoto hao iliwaweze kuchukua watoto wengi zaidi wakiwemo watoto wa mbali na mazingira hayo, pia usafiri kwa watoto hao wanaotoka mbali huku elimu itolewe zaidi katika jamii juu yakuwahudumia watoto hao yatima katika maeneo yao.

Taasisi ya SOS Children Village iliaanzishwa mwaka 1984 huko Zanzibar na baadae kufungua vituo vingine vinne katika mikoa ya Mwanza,Dar es Salaam, Arusha na Iringa, hadi sasa imeshaeenea katika nchi mbalimbali kama South Afrika na Uganda.
Katibu Tawala Richard Kwitega, akimsikiliza mmoja wa vijana aliyelelewa na kituo cha SOS Children Village Bi. Anna Lomayani na sasa anafamilia yake.

Bwana Kwitega, akiwasalimia baadhi ya watoto wa shule ya awali wa kituo cha SOS Children Village.