RC Akiapishwa

Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Mhe. Mrisho Gambo.

Ziara ya Waziri Mkuu wa Tanzania

Mhe. Mrisho Gambo akiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa Ofisini kwake, Jijini Arusha.

JPM ,Mrisho Gambo Picha ya Pamoja

Dk. John Pombe Magufuli akipiga picha ya pamoja na mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.

Samia Suluhu Hassan akiwasili Jijini Arusha

Mkuu wa Mkoa Arusha, Mhe Mrisho Gambo Akimpokea Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Picha ya Pamoja

Mhe. Mrisho Gambo akiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa.

Wednesday, October 26, 2016

GAMBO ASHIRIKI UJENZU WA DARAJA FUPIMkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Mashaka Gambo ameshiriki ujenzi wa daraja fupi(drift) katika kijiji cha Orgirah kata ya Mundarara na tarafa ya Engarenaibow kwa lengo lakuhamasisha wananchi na viongozi wengine.

Akitoa msisitizo kwa viongozi kujitoa sana pale wanapoitajika kushiriki shughuli mbalimbali za  maendeleo kwa wananchi wao hasa zile ambazo zimeanzishwa kwa nguvu za wananchi wenyewe.

“Viongozi mbalimbali wasiwe wazito kujitoa katika shughuli kama hizi za maendeleo ya wananchi na hasa ambazo zimeanzishwa kwa nguvu za wananchi wenyewe nivema basi na serikali nayo kupitia viongozi kwa ngazi tofauti kujitokeza nakuunga mkono”.

Mradi huo wa daraja fupi(drift) ulianza rasmi mnamo Octoba ,2016 kwa lengo lakuunganisha vijiji viwili vya Orgirah na Igulailungwa ambavyo vilitenganishwa kwa ukosefu wa daraja hilo fupi na kupelekea kwa vijiji hivyo kukosa mawasiliano.

Aidha mradi huo mpaka kukamilika utagharimu kiasi cha shilingi milioni 9 ambapo mpaka sasa ni milioni 6 tu ndio zimetumika katika ujenzi huo, ikiwa Halmashauri ya Wilaya ya Longido ilichangia 450,000, Mkurugenzi wa halmashauri alichangia 640,000 na nguvu za wananchi ni milioni 5.

Hata hivyo Gambo aliwapongeza wananchi hao kwa juhudi walizozianza za ujenzi huo na hivyo serikali itawasaidia pale penye mapungufu na wananchi wenyewe wanatakiwa kujitokeza zaidi hususani kwenye shughuli kama hizo za maendeleo.

Mradi huo bado unamapungufu ya shilingi milioni 2 ili kukamilisha milioni 9 kama gharama nzima ya ujenzi na Mkuu wa Mkoa aliaidi kuchangia mifuko 30 ya simenti,pesa taslimu 500,00 na kutoa katapila ikiwa wananchi watakuwa tayari kuchangia mafuta. 
Meneja wa TANROAD Arusha Enginia John Kalupale aliaidi kuchangia mifuko 50 ya simenti.

Pia mwenyekiti wa chama cha CCM Mkoa Lekule Ole Laiza atachangia mifuko 30 ya simenti, mwenyekiti wa Halmashauri ya Longido bwana Sabore Molleiment atachangia 500, 000, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Longido  Juma Muhina nae atachangia 400,000 na Halmashauri yenyewe itaenda kujadili kwenye vikao vyake namna yakusaidia ujenzi huo.

Gambo bado yupo ziarani Longido huku akishirikiana na wananchi wa Wilaya hio katika shughuli mbalimbali za maendeleo yao.


Wananchi wa kijiji cha Orgirah wakishiriki katika ujenzu wa daraja fupi(drift) kwenye kijiji chao.

Hili ndilo daraja fupi(drift) lililoanzishwa kwa nguvu za wananchi wa kijiji cha Orgirah kata ya Mundarara Wilayani Longido.

Tuesday, October 25, 2016

Mtendaji wa Kata awekwa chini ya ulinzi wa polisiMkurugenzi halmashauri ya Longido bwana Juma Mohamed Muhina ameamuru kukamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi  mtendaji wa kata ya Egirai Lumbwa Wilayani Londigo bwana Paulo Luka kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha za ujenzi wa madarasa ya shule ya sekondari  Natroni Flamingo.

Maamuzi hayo yamefikiwa baada ya wananchi wa kijiji cha Meligoi kata ya Egirai Lumbwa kuikata taarifa iliyosomwa na mtendaji wa kata hiyo iliyoonyesha ujenzi mpaka kukamilika utagharimu kiasi cha milioni 50 lakini michango ya awali ilikuwa milioni 12 na kati ya hiyo  milioni 4 tu ndio ilikuwa michango ya wananchi.

Wananchi hao walimweleza Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo  aliyekuwa akisikiliza Changamoto mbalimbali walizonazo baada yakufanya ziara katika kijiji hicho , walisema kuwa wao wanavyojua wamechanga zaidi ya fedha zilizotajwa  kwenye taarifa hiyo.

Hivyo Gambo alimtaka Mkaguzi wa ndani wa Halmashauri kufafanua juu ya matumizi ya fedha hizo, akifafanua Bi.  Mwajuma mdaira alisema alifanya ukaguzi na kugundua kuwa fedha zilizokusanywa kwa njia ya michango ilikuwa milioni 95 na milioni 50 kati ya hizo zilitumika kwenye marekebisho ya majengo ya shule japo hakukuwa na mikata yoyote iliyoingiwa kati ya shule na mkandarasi.

Pia fedha hizo zilitumika bila kutumia stakabadhi za malipo za halmashauri, na kuna wawekezaji 2 ambao ni Winget Windros Safari walichangia mifuko 200 ya simenti na mingine 200 ilitolewa na Kilomberong Hunting kusaidia ujenzi lakini mifuko 144 kati ya hiyo iliuzwa na fedha zake hazikujulika matumizi yake lakini bado anaendelea na ukaguzi zaidi.

Hivyo kumpelekea Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo kutaka kufahamu hatma ya mtendaji huyo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri aliyekili kupata taarifa hiyo jana yake tu na hapo hapo akamuamuru kamanda wa polisi Wilaya kumkamata mtendaji huyo nakumpeleka kituoni kwa maelezo na upelelezi zaidi juu ya ubadhilifu huo.

Mkuu wa Mkoa, Mrisho Gambo yupo katika ziara ya kikazi Wilayani Longido kwa mda wa siku 5 ilikujionea maendeleo na pia kusiliza Changamoto mbalimbali za wananchi wa Wilaya hiyo.

 

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Meligoi walioikata taarifa ya mtendaji wa kata yao, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo(hayupo pichani) katika mkutano wa hadhara, kijiji hapo.

Saturday, October 22, 2016

Wilaya ya Ngorongoro yapata neema kubwa
Rais Dkt John Pombe Magufuli ameandika historia kwa wananchi tangu Tanzania ipate uhuru na tangu atimize mwaka 1 madarakani kwa kuipatia Wilaya ya Ngorongoro  barabara ya lami yenye urefu wa kilomita 60 tangu Wilaya hiyo ianzishwe.

Haya yameelezwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo wakati wa Kikao cha 38 cha bodi ya barabara cha Mkoa huo.

Gambo alisema  barabara hiyo inayotarajiwa kuanza kujengwa kwa kiwango cha lami  na itaunganisha  mji wa Wasso hadi Sale kilomita 60 imepata Baraka zote kutoka kwa Rais Magufuli.

Gambo ameeleza katika Kikao  hicho kwamba  Rais Magufuli ameagiza kuanza kujengwa kwa barabara hiyo mara moja  kwa kiwango cha lami kama alivyoahidi wakati wa Kampeni alipokuwa katika Wilaya hiyo.

Amesema barabara hiyo  inatarajiwa kutekelezwa na Wakala wa barabara mkoani Arusha ( TANROADS).

Mkuu huyo wa Mkoa amesema  hii ni hatua muhimu sana kwa Wananchi wa Wilaya ya Ngorongoro ,Wilaya  haina hata barabara moja yenye kiwango cha lami.

Mkuu huyo wa Mkoa pia alisema  fedha zinazotolewa na wafadhili benki ya dunia  sio msaada  bali ni fedha za mkopo kwa Tanzania ambazo  Tanzania italazimika kuzilipa hapo baadaye.

Akitoa shukrani zake mbunge wa jimbo la Ngorongoro Tate William Ole Nasha alisema kwa mala ya kwanza Ngorongoro inapata barabara yenye kiwango cha lami, kweli itakuwa furaha kubwa sana kwa wananchi wa Wilaya hito.

Wilaya ya Ngorongoro ni kati ya Wilaya sita za Mkoa wa Arusha  ambapo Wilaya hii inakabiliwa na matatizo makubwa ya miundo mbinu ya ukosefu wa barabara za uhakika ambapo usafiri katika Wilaya hiyo ni wa kubahatisha kutokana na kukosekana kwa miundo mbinu ya uhakika ya barabara kwenda maeneo ya vijijini.

Hivi sasa TANROADS inahudumia kiasi cha kilomita 1,220 katika Wilaya   za Mkoa wa Arusha zikiwemo  barabara kuu na barabara za Mkoa alisema Meneja wa Mkoa Mhandisi  John Kalupale.


Wajumbe wa bodi ya barabara  ya Mkoa wa Arusha wakisikiliza agenda mbalimbali zikijadiliwa za kikao cha 38 cha bodi hiyo.

KAMPUNI YA UKANDARASI KUTOKA KOREA YATOA MSAADA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Mashaka Gambo amepokea mifuko 500 ya simenti na mabati 500 kutoka kwa kampuni ya ukandarasi ya Hanil JV Jiangsu kutoka Korea inayojenga barabara ya Tengeru Sakina.
Msaada huo umetolewa ofisini kwake ambapo tukio hilo limeweza kushuhudiwa na viongozi mbalimbali wa Mkoa,Wilaya na Wabunge wa viti maalumu wa Mkoa wa Arusha.
Akipokea msaada huo,Mrisho Gambo amesema atagawa mifuko 100 ya simenti na mabati 100 kwaajili ya ujenzi wa Zahanati kata ya Murieti kwasababu kumekuwa na ongezeko kubwa sana la wagonjwa katika hospitali ya Mkoa Mt.Meru wanaotoka maeneo hayo hivyo ujenzi huo utasaidia  kupunguza wagonjwa katika hospitali hiyo.
Pia yatakayo baki atayapeleka Wilaya ya Longido katika kusaidia ujenzi wa bweni la shule ya sekondari Longido ambayo liliungua moto nakuteketeza kila kitu.
“Napenda kuishukuru na kuipotengeza kampuni ya ukandarasi ya barabara ya Tengure Sakina na ile ya njia mbadala(by path) kwakutoa msaada huu na kwakuwa tumeshaanza  mkakati wa ujenzi wa madara kwa shule za msingi na Sekondari,hivyo nitagawa hayo mifuko ya simenti 100 na mabati 100 ikajenge Zahanati kata ya Murieti na yaliyobaki yataenda Longido katika ujenzi wa bweni lililoungua”.
Mkurugenzi  Mtendaji wa kampuni ya ukandarasi ya Hanil JV Jiangsu bwana Xie Jianbao amesema kampuni yao imetoa msaada huo ikiwa ni moja ya shughuli zao zakusaidia jamii katika shughuli mbalimbali za maendeleo.
“Tumetoa mifuko ya simenti 500 na mabati 500 kama moja ya mchango wetu katika kusaidia jamii yetu kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo”.
Aidha Mkurungezi wa Jiji la Arusha,Athumani Kihamia alisema  kutokana na wingi wa wananchi waliopo katika kata ya Murieti Zahanati hiyo itaenda kuwasaidia sana na kwakipindi kisichozidi miezi 2 Zahanati hiyo itakamilika na wananchi wataweza kuitumia.
Ukosefu wa kituo cha afya katika kata ya Muriet ulibainika baada ya Mkuu wa Mkoa Gambo kufanya ziara katika kata hiyo nakupata malalamiko kutoka kwa wananchi kuwa wanatembe umbali mrefu sana kutafuata huduma za afya.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akitoa shukrani kwa kampuni ya ukandarasi ya Hanil JV Jiangsu kwa kutoa msaada wa mifuko ya simenti 500 na mabati ya 500 kwa shughuli za maendeleo za Mkoa wa Arusha.

Thursday, October 20, 2016

Mhe.Waziri Mkuu Kassim Majaliwa apokea mifuko 900 ya simenti kutoka NSSF.

Waziri Mkuu wa Jamuhuli ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akipokelewa na Waziri wa Nchi, ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na wenye ulemavu, Jenista Mhagama alipowasiri katika uwanja wa Kisongo Jijini Arusha.

Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea mfuko wa simenti kutoka kwa mwenyekiti wa bodi ya NSSF Prof. Samweli Wangwe,ambapo NSSF wamechangia mifuko 900 kwa wahanga wa tetemeko Kagera.

Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa pamoja na viongozi mbalimbali katika mkutano mkuu wa mwaka wa shirika la hifadhi ya jamii(NSSF) katika ukumbi wa AICC,Jijini Arusha.

Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali(kulia kwake) Mhe. Jenista Mhagama na (kushoto kwake) Mhe. Mrisho Gambo Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Jijini Arusha.

Kikao cha wafanyabiashara,Jijini Arusha.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo,akizungumza na wafanyabiashara wa Mkoa wa Arusha, alipokutana nao jijini Arusha.


Baadhi ya wafanyabiashara wa Mkoa wa Arusha wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Arusha(hayupo pichani)alipoitisha mkutano wakuzungumza nao,jijini Arusha.

Tuesday, October 18, 2016

MKUU WA MKOA WA ARUSHA MRISHO GAMBO AZINDUA UJENZI WA HOSPITALI YA MAMA NA MTOTO.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Mashaka Gambo akizundua rasmi ujenzi wa hospitali ya mama na mtoto,itakayojengwa katika eneo la Burka Wilayani Arumeru,jijini Arusha,pembeni yake(kulia) Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Alexander Mnyeti na upande wa (kushoto mwanzo)Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema wakishuhudia uzinduzi huo.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,alielezea historia fupi la mradi wa ujenzi wa hospitali ya mama na mtoto,Wilayani Arumeru.

Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhulia uzinduzi wa ujenzi wa hospitali ya mama na mtoto, Burka jijini Arusha.