RC Akiapishwa

Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Mhe. Mrisho Gambo.

Ziara ya Waziri Mkuu wa Tanzania

Mhe. Mrisho Gambo akiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa Ofisini kwake, Jijini Arusha.

JPM ,Mrisho Gambo Picha ya Pamoja

Dk. John Pombe Magufuli akipiga picha ya pamoja na mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.

Samia Suluhu Hassan akiwasili Jijini Arusha

Mkuu wa Mkoa Arusha, Mhe Mrisho Gambo Akimpokea Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Picha ya Pamoja

Mhe. Mrisho Gambo akiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa.

Thursday, November 24, 2016

Gambo akutana na Kamishina Mkuu wa Uingereza

Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Mashaka Gambo akizungumza na Kamishina Mkuu wa Uingereza Sarah Cooke alipomtembelea ofisini kwake jijini Arusha.


Mkuu wa Mkoa wa Arusha akiwa kwenye picha ya pamoja na Kamishina Mkuu wa Uingereza Sarah Cooke,jijini Arusha.

ZAIRA YA SAMIA SULUHU HASSANI KATIKA KIWANDA CHA MT,MERU MILLERS

Makamu wa Rais,Samia Suluhu Hassan akisikiliza maelezo ya malighafi inayotumika katika kutengenezea mafuta yatokanayo na alizeti katika kiwanda cha Mt. Meru Millers, jijini Arusha.

Makamu wa Rais,Samia Suluhu Hassani ametembelea kiwanda cha Mt. Meru Millers Limited  cha jijini Arusha kinachojishughulisha na utengenezaji wa mafuta yatokanayo na alizeti.

Akizungumza baada yakujionea uzalishaji wakiwanda hicho,amesema lengo kubwa ya ziara yake katika kiwanda hicho ilikuwa nikujionea shughuli zinazofanywa na kiwanda hicho.

Pia ameweza kusikiliza changamoto mbalimbali zinazozikabili kiwanda hicho na kubwa ikiwa ni utozwaji wa kadi nyingi na serikali itahakikisha kunakuwa na utaratibu mzuri wa ulipaji wa kodi hizo.

Aidha alisisitiza zaidi kuwa serikali ya awamu wa tano imedhamilia ujenzi wa viwanda vingi nchini ambavyo vitatumia malighafi za ndani ya nchi nakukuza uzalisha kwa wakulima na hata pia kutoa ajira za kutosha.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mt. Meru Millers Atul Mittal alisema ikiwa serikali itapunguza kodi hizi nyingi itasaidia ukuwaji wa viwanda vilivyopo na hata kuhamasisha wawekezaji wengine kuwekeza kwenye viwanda hapa nchini.

Makamu wa Rais yupo Mkoa Arusha kikazi kwa mda wa siku 3 ambapo atendelea kutembelea viwanda vya mkoani  hapa na pia atazindua jengo la Mahakama ya Afrika.
Makamu wa Rais,Samia Suhulu Hassan akiangalia moja ya kifungashio cha mafuta ya alizeti kilichotengenezwa na kiwanda cha Mt,Meru Millers,Arusha.

Makamu wa Rais,Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Mkoa na wafanyakazi wa kiwanda cha Mt.Meru Millers,jijini Arusha.

Sunday, November 20, 2016

UMILIKI WA SHAMBA LA MANYARA RANCH KURUDISHWA CHINI YA HALMASHAURI YA MONDULI

Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Mashaka Gambo akihutubia wananchi wa kijiji cha Esilalei katika tarafa ya Makuyuni Wilayani Monduli.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo ameiagiza halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha kupitia upya taratibu na kanuni zilitumika kwenye umiliki wa shamba la Manyara Ranch lililopo tarafa ya Makuyuni.

Alisema hayo alipofanya ziara ya siku moja katika tarafa hiyo nakutembelea shamba la Manyara Ranch ambalo wananchi wanadi ni mali yao baada ya umiliki wake kufutwa mwaka 1999 nakurudishwa kwa wananchi.

Hata hivyo bado kuligubikwa na maswali mengi ya hati miliki ya shamba kuandikwa jina la Tanzania Land Conversation Trust (TLCT)  ambacho ni chombo cha kusimamia shamba hilo na badala ya mmiliki mkuu ambae ni Halmshauri ya Wilaya ya Monduli, hali iliyopelekea Gambo kutolea maamuzi ya hati miliki iandikwe Halmashauri ya Wilaya ya Monduli.

“Naiagiza Halmashauri kuhakikisha hati miliki ya shamba hili isomeke jina la Halmashauri badala ya TLCT kwasababu tayari shamba lilisharudishwa kwa wananchi na halmashauri ndio msimamizi wa mali za wananchi”,alisema.

Akisoma taarifa fupi ya shamba la Manyara Ranch Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya African Wildlife Foundatio(AWF)ambao ndio wanaendesha shughuli zote katika shamba hilo bwana Fidelisi Ole Kashe amesema taasisi hiyo iliingia mkataba wakuendesha shughuli zote ndani ya shamba kutoka kwa TLCT baada ya chombo hicho kushindwa kuziendesha.

Aidha akifafanua zaidi Mkurugenzi mtendaji wa TLCT bwana Boniface Ngimojiro alisema TLCT iliundwa na bodi ya halmashauri ya wilaya ya Monduli ili isimamie na kuendesha shughuli zote za shamba la Manyara Ranch na baada yakushindwa kuendesha ndipo wakazikabidhi kwa AWF.

Hata hivyo Gambo alisema ataunda timu yakuchunguza shughuli zote za TLCT kwa mda wa miaka 10 ya nyuma ilikusaidia kufahamu zaidi kama chombo hicho bado kinahitajika katika uwendeshaji na usimamizi wa shughuli za shamba la Manyara Ranch.

Gambo amekuwa akifanya ziara zake katika wilaya mbalimbali za Mkoa wa Arusha kwa lengo lakusikiliza kero mbalimbali za wananchi zinazowakabili.

Mkurugenzi Mtendaji wa AWF akisoma taarifa fupi ya mradi wa shamba la Manyara Ranch kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo(hayupo pichani),pembeni yake (kulia) ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha,Richard Kwitega akifuatilia taarifa hiyo.

Wananchi wa kijiji cha Esilalei wakiwa kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akijibu hoja mbalimbali za wananchi wa Makuyuni alipofanya ziara katika tarafa hiyo iliyopo Wilayani Monduli.

Wednesday, November 16, 2016

CHAMA CHA WAMILIKI WA MAGARI YA NOAH WAKABIDHI SIMENTI MIFUKO 200

Mkuu wa Mkoa, Mrisho Gambo akipokea mifuko 200 ya simenti kutoka kwa chama cha wa wamiliki wa magari aina ya Noah cha Jijini Arusha.

Mkuu wa Mkoa, Mrisho Gambo akipokea mifuko 200 ya simenti kutoka kwa chama cha wa wamiliki wa magari aina ya Noah cha Jijini Arusha.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo akimkabidhi mifuko 50 ya simenti Mkuu wa Wilaya ya Longido Daniel Chongolo kwaajili ya ujenzi wa kitua cha afya Namanga, Wilayani Longido.

TAARIFA YA MRADI WA PAMOJA TUWALEE

Katibu Tawala wa Mkoa,Richard Kwitega akitoa shukrani baada yakukabidhiwa mradi wa Pamoja Tuwalee,ofisini kwake Jijini Arusha.

Wajumbe wa kamati ya Pamoja Tuwalee kwa ngazi ya Mkoa, waliofika kukabidhi mradi wao kwenye ofisi ya RAS Arusha.Friday, November 4, 2016

Matokeo ya darasa la saba 2016