Saturday, March 25, 2017

SIKU YA KUDHIBITI UGONJWA WA KIFUA KIKUU.

Waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto,Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) juu ya maadhimisho ya siku yakudhibiti ugonjwa wa kifua kikuu.


Waziri wa Afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoo,Ummy Mwalimu amezindua mashine zakisasa (molekyula) zakupima ugonjwa wa kifua kikuu ambazo zitatumika katika hospitali zote za rufaa nchini na ikiwa ni siku yakudhibiti ugonjwa wa kifua kikuu duniani.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwa mkuu wa mkoa wa Arusha nakusisitiza kuwa mashine hizo  zinauwezo wakupima wagonjwa 12 kwa siku na zinauwezo wakugundua usugu wa dawa aliyonao mgonjwa nakupima virusi vya UKIMWI.

Changamoto kubwa ambayo wizara ilikuwa inapata nikuwagundua wagonjwa wa kifua kikuu mapema nahii imetokana na wagonjwa wengi kuwa na usugu wa dawa walizokuwa wakitumia na hivyo kuwafanya wasipone kwa wakati.

Kwa mujibu wa taarifa ya shirika la afya dunia Tanzania inawagonjwa takribani 1060 wanaougua ugonjwa wa kifua kikuu kila mwaka na asilimia 30 kati ya wagonjwa 100 tu ndio wanaofika katika vituo vyakupatiwa tiba.

Mkoa wa Dar es Salaama ndio unaongoza kuwa na wagonjwa wengi wa kifua kikuu takribani asilimia 22 ikifuatiwa na mikoa ya Mwanza,Mbeya,Morogoro,Shinyanga,Arusha,Mara,Manyara,Tanga na Kilimanjaro ambayo yenyewe inachangia asilimia 63 ya wagonjwa wote kwa wagonjwa waliogundulika mwaka 2015.

Mpaka sasa wizara imenunua mashine 70 ambazo wanatarajia kuzisambaza katika hospitali zote za rufaa za mikoa ikiwa ni awamu ya kwanza na pia wanampango wakuongeza mashine hizo hadi kufikia 150 ili waweze kubaini wagonjwa wengi zaidi na hata wale wenye kifua kikuu sugu.

Amesema kutokana na taarifa ya shirika la afya duniani ya mwaka 2016 Tanzania kila mwaka inashindwa kuwafikia wagonjwa takribani 2400 wenye kifua kikuu sugu na laki moja wenye kifua kikuu.

Hivyo amezitaka halmashauri kuweka mikakati yakubaini wagonjwa wote wa kifua kikuu kwa kuhakikisha kuwa pindi mgonjwa anapoletwa hospitali halmashauri ifikie ile kaya ambayo mgonjwa umetoka ili kuwapima wakazi wote wa kaya hiyo kama kuna ambae ameambukizwa.

Pia amepiga marufuku kwa shule zote za bweni kupokea mwanafunzi yoyote bila kuwa na fomu maalumu yakutoka hospitali inayoonyesha vipimo vya magonjwa mbalimbali ambayo mwanafunzi huyo amepimwa ikiwemo ugonjwa wa kifua kikuu.

Aidha ameagiza wagonjwa wote waliopo kwenye kundi hatarishi hasa wenye virusi vya UKIMWI, watoto walio chini ya amri wa miaka 5,wamama wajawazito,wazee,wafungwa, watumiaji wa madawa ya kulevya,watu wenye kisukari na saratani ni lazima wachunguzwe ugonjwa wa kifua kikuu mara tu wanapofika kwenye vituo vya tiba.

Pia kundi linguine litakalopimwa ugonjwa huu ni wagonjwa wanaofika katika idara za nje,cliniki za watu wenye virusi vya UKIMWI na wagonjwa wote watakaokuwa wamelazwa kwenye hospitali za serikali.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo nae amemwahidi Waziri Ummy kuongeza ushirikiano katika kupambana dhidi ya ugonjwa huu wa kifua kikuu kwa  kushirikiana na wilaya zote  za mkoa kuhakikisha kuwa kila kijiji na mtaa kwenye mikutano yao mikuu ya hadhara watoe elimu ya kutosha na kuhamasisha wananchi wakapime afya zao kwenye vituo vya afya.

Wizara ya afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto kila mwaka imekuwa ikiadhimisha siku ya kudhibiti ugonjwa wa kifua kikuu na mwaka huu siku hiyo ameadhimisha rasmi mkoani Arusha.


0 comments:

Post a Comment