Wednesday, December 20, 2017

Shule binafsi za Sekondari zatakiwa kufuata sheria ya elimu.

Katibu Tawala Msaidizi upande wa elimu akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani)juu ya usimamizi wa sheria ya elimu kwa shule binafsi.


Shule zote binafsi za mkoa wa Arusha zimetakiwa kufuata sheria  ya elimu ya mwaka  2012 ya usimamizi wa upandaji wa madarasa  kwa wanafunzi wa shule hasa  za Sekondari.

Akitoa rai hiyo katibu tawala masaidizi upande wa elimu bwana Gift Kyando, amesema serikali  imeweka utaratibu wa upimaji wa wanafunzi kwa darasa la nne, darasa la saba,kidato cha pili na kidato cha nne.

“Hakuna utaratibu wakumpima mwanafunzi wa kidato cha tatu kwenda kidato cha nne kama inavyofanywa na baadhi ya shule binafsi kwa kuweka wastani wa alama za masomo kwa wanafunzi na ambae hata fikisha kiwango hicho hufukuzwa shule au kuamliwa kurudia kidato”.

Amesema serikali haitafumbia macho kwa shule yoyote itakayokiuka sheria hiyo ya elimu nakuwataka wakuu wote wa shule wanaoendesha shule zao kwa kukiuka utaratibu huo kuacha mara moja na pia amewasihi wazazi wote waendelee na maandalizi ya watoto wao wanaoingia kidato cha nne bila hofu yoyote.

Pia amesema serikali itaendelea kuzifuatilia shule zote za binafsi hasa zilizobainika kukiuka sheria hiyo ili kuhakikisha wanafunzi hawafukuzwi au kurudia madarasa bila utaratibu uliowekwa na serikali.

Amewataka wazazi wote ambao watoto wao watakataliwa kuendelea na masomo kwa kigezo cha kikosa wastani wa alama za shule husika, watoe taarifa haraka katika ofisi za elimu za  mkoa wa Arusha  kwa hatua zaidi.

0 comments:

Post a Comment