Friday, April 13, 2018

TUTAENDELEA KUENZI MAZURI YA SOKOINE-MAJALIWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa akisalimia na mke mkubwa wa marehemu Sokoine Bibi Napono Sokoine alipowasiri nyumbani kwa hayati Sokoine alipohudhuria misa ya kumbukumbu cha kifo chake,pembeni ni mke wa pili wa marehemu Bibi Nekiteto Sokoine,Wilayani Monduli.

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, amesema serikali ya awamu ya tano inaendelea kuenzi   juhudi zilizofanywa na hayati  Edward Sokoine ya kupambana na uhujumu uchumi katika nchi.

Ameyasema hayo alipohudhuria ibada ya kumbukumbu ya kifo cha hayati Edward Moringe Sokoine nyumbani kwake wilayani Monduli.

Amesema hayati Edward Moringe Sokoine alikuwa  mkweli na mwadilifu katika utumishi wake na kwa jamii yake,hivyo sisi kama viongozi wa awamu hii ya tano hatuna budi kuendelea kuiga mfano wake.

“Jukumu letu nikuendelea kumuombea hayati Sokoine kwani matendo yake bado tunayaishi na yataendelea kutuongoza.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha maombelezo cha kumbukumbu ya kifo cha hayati Edward Moringe Sokoine nyumbani kwake Monduli.

Serikali hii inaendelea kuthamini dira za viongozi waliotangulia kwa kuhakikisha mali za nchi zinawanufaisha watanzania wote.

Amesisitiza kuwa hayati Sokoine alijikita katika kuwajibika kwa watumishi wa umma na serikali ya awamu hii nayo imeweza kurudisha nidhamu na uwajibikaji kwa watumishi wa umma.

Pia hayati Edward Sokoine alianzisha falsafa ya ‘Kilimo ni uti wa Mgongo’ na sasa serikali inaendeleza falsafa hiyo kwa kujikita katika kilimo cha uzalishaji chenye tija.

Amesisitiza  kuwa hayati Sokoine  alikuwa msikivu kwa kusikiliza kero mbalimbali za watu na hakuwa na kinyongo wala tabia ya kujilimbikizia mali hivyo ni mfano wakuingwa na watanzania wote.

Waziri Mkuu Kassim Majali akiwaongoza baadhi ya viongozi katika misa ya kumbukumbu ya kifo cha hayati Edward Sokoine iliyofanyika nyumbani kwake Monduli.

 Askofu mstaafu wa jimbo kuu katoliki la Arusha mhashamu Josephati Luis Lweburu akiendesha ibada hiyo amesema hayati Edward Sokoine alikuwa mcha Mungu sana ndio kukamfanya awe mwaminifu na muwajibikaji katika utumishi wake.

Amesema alikuwa mtu wakubuni mbinu mbalimbali za kusaidia watu wake katika jamii yake na hii imesababisha kuendelea kukumbukwa na wengi kwa upendo wake huo.

Akitoa neno la shukrani Lembrisi Kivuyo kwa niaba ya familia ya hayati Edward Moringe Sokoine,amesema serikali imekuwa ikiwa karibu sana na familia hiyo tangu kuondokewa na mpendwa wao hivyo ameishukuru sana serikali kwa hilo.

Amesema familia yao itaendelea kuunga mkono serikali ya awamu ya tano kwa juhudi zake zinazofanya katika kuleta maendeleo kwa nchi.

Hayati Edward Moringe Sokoine alifarikia Aprili 12, 1984 akiwa kama waziri 
mkuu wa Tanzania wa tatu akimfuatia hayati Rashidi Mfaume Kawawa na kila mwaka familia yake hufanya ibada hiyo ya kumbukumbu.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa na viongozi wa dini  mbele ya kaburi la hayati Edward Moringe Sokoine alipoweka shada la mauwa katika ibada ya kumbukumbu ya kifo chake,mkoani Arusha.


0 comments:

Post a Comment