Monday, April 9, 2018

WATANZANIA DUMISHENI AMANI-MAGUFULI

Watanzania wote nchini wametakiwa kuendelea kudumisha amani na mshikamano katika maeneo yao ili kukuza maendeleo ya uchumi kwa nchi.

Yamesemwa hayo na Rais wa jamuhuli ya muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli alipohudhuria sherehe za kusimikwa kwa askafu mkuu wa jimbo la Arusha mhashamu Isaac Imani.

Amesema amani ndio kitu pekee kitakachoweza kuleta mshikamano,upendo na maendeleo katika nchi yetu.

Watanzania wote wanapaswa kufahamu kuwa amani ndio kitu wanachotakiwa kukitunza na kukiheshimu,hivyo wasikubali baadhi ya watu wawashawishi kuipoteza amani hiyo.

Serikali itaendelea kushirikiana na viongozi wa dini na madhehebu yote ya hapa nchini katika kudumisha amani na kuleta maendeleo ya nchi kwani serikali haina dini na inahudumia watu wake wote.

Aidha, katika kuendeleza ujenzi wa kanisa jipya la jimbo la Arusha ameaidi kuchangia mifuko 300 ya simenti,pia ametoa zawadi ya Ng’ombe 2 kwa askofu aliyemaliza mda wake  Josephati Luisi Lweburu kama ishara yakumshukuru kwa ushirikiano wake kwa serikali.

Akisisitiza zaidi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amewataka wananchi wa Arusha waendelee kufuata sheria na taratibu za nchi,hii itasaidia kuepuka migongano ya hapa na pale inayojitokeza mara kwa mara.

Alimshukuru askofu aliyemaliza mda wake wa utumishi askofu Josephati Lweburu kwa ushirikiano wake mkubwa aliouwonyesha kwa uongozi wa mkoa.

Askofu mpya Isaac Amani amesema uongozi ni dhamani inayoitaji mshikamano baina ya wanaoongozwa na wanaoogonza.

Amesema ushirikiano na kusikilizana ndio itasaidia kufanya kazi kwa bidii na kwa umoja.

Aidha, amesema kama nchi tusiruhusu ufa wowote katika nchi yetu bali tukae kwa upendo na amani.

Magufuli alihudhuria sherehe za kusimikwa kwa askofu mkuu wa jimbo la Arusha mhashamu Isaac Amani baada ya aliyekuwa askofu wa jimbo hilo Josephati Lweburu kumaliza mda wake wa utumishi.

Rais Magufuli akiwa na mkwe Mama Janeth wakiwasamilia baadhi ya maaskofu na Mapadre walipohudhuria sherehe za kusimikwa kwa askofu mkuu wa jimbo katoriki la Arusha mhashamu askofu Isaac Imani.


Rais Magufuli akimpongeza askofu mkuu wa jimbo katoriki la Arusha mhashamu Isaac Imani baada yakusimikwa rasmi kuwa askofu wa jimbo la Arusha,katika Kanisa la Mt.Theresia jijini Arusha.


Mke Rais Magufuli, mama Janeth Magufuli akimpa mkono wa hongera askofu mteule wa jimbo kuu katoriki la Arusha mhashamu Isaac Imani baada yakusimikwa rasmi katika kanisa la Mt. Theresia jijini Arusha.


0 comments:

Post a Comment