Friday, September 14, 2018

MILIONI 469 ZATUMIKA KATIKA UJENZI WA KITUO CHA FYA

Jengo la kituo cha afya kata ya Mto wa Mbu wilayani Monduli,kilichojengwa na serikali kwa kushirikiana na nguvu za wananchi.Milioni 469 zimetumika katika ujenzi wa kituo cha afya Mto wa Mbu wilayani Monduli.

Akisoma taarifa ya mradi huo Mganga mkuu wa kituo cha afya Dr. Emma Agostino Msofe, amesema ujenzi wa kituo hicho ulianza mwaka 2017 baada ya serikali kutoa fedha kiasi cha shilingi milioni 400.

Pia fedha nyingine zimetoka halmashuri kiasi cha shilingi milioni 30 na wananchi  wamechangia milioni 39.

Ujenzi wa kituo hicho cha afya unaendelea na mpaka sasa majengo yaliyojengwa ni  jengo la upasuaji, jengo la wazazi,jingo kufulia,nyumba ya utumishi,vyoo vya nje na matenki ya kuhifadhia maji.

Amesema kituo hicho cha afya kitawasaidia wananchi kupata huduma bora za afya na katika mazingira bora.

Nae kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa ndugu. Charles Francis Kabeho, amesema wananchi wanatakiwa kukitunza kutuo hicho kwa umakini na pia amewataka watumishi watoe huduma bora na kwa weridi kwa wananchi.


Mwengi wa Uhuru ulianza mbio zake mkoani Arusha Mnamo Septamba 12 katika wilaya ya Ngorongoro kisha wilaya ya Karatu na sasa unaendelea katika wilaya ya Monduli.

Kiongozi wa mbio za Kitaifa ndg. Charles Francis Kabeho, akizundua kituo cha afya cha Mto wa Mbu wilayani Monduli.


Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Charles Kabeho ( mwenye sare ya gwanda) akiwa na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Monduli wakitoka kizindua mradi wa kituo cha afya cha mto wa Mbu.


Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Charles Kabeho akikagua mradi wa kuchakata chakula cha mifugo klatika kijiji cha Mungere kata ya  Esilalei wilayani Monduli.


0 comments:

Post a Comment